Pata taarifa kuu
TUNISIA

Chama tawala nchini Tunisia kuzungumza na vyama vya wafanyakazi kutafuta suluhu ya mgogoro ulipo nchini humo

Tunisia inatarajia kufanya tena mazungumzo kwa ajili ya kutafuta suluhu la mzozo wa kisiasa uliosababishwa na kuuawa kwa Mwanasiasa wa upinzani mwezi uliopita, huku mazungumzo hayo yakiwa hayana dalili ya kufikiwa kwa mwafaka. Mazungu ya awali yalishindwa kufikia muafa, na sasa awamu nyingine imeandaliwa kutafuta suluhu ya matatizo yaliopo.

REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Chama Tawala cha kiislamu nchini humo, Ennahda kinatarajia kufanya mazungumzo na shirikisho la Wafanyakazi nchini humo kutafuta suluhu la mgogoro wa Tunisia uliodumu kwa majuma kadhaa.

Maswala kadhaa yaliibuka kwenye mkutano uliopita, lakini mwishoni mwa juma Chombo cha chama hicho kinacho husika na maswala ya maamuzi kilisema kuwa kinaidhinisha ombi la Kiongozi wa Chama hicho, Rashed Ghannouchi aliyeoomba kuwepo na Serikali ya umoja na kukataa mapendekezo ya upinzani kuunda Serikali ya Watu wenye utaalam mbalimbali wasio wanasiasa.

Wanaharakati wa upinzani wanadai Serikali inayoongozwa na ennahda ijiuzulu, serikali ambayo imekua wakiishutumu kukandamaiza haki za Wanawake na kushindwa kupambana na makundi ya kiislamu yenye msiamamo mkali makundi ambayo yanashutumiwa kumuua Mwanasiasa wa upinzani, Chokri Belaid.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.