Pata taarifa kuu
TUNISIA

Maandamano yaendelea nchini Tunisia kuitaka serikali kujiuzulu

Maandamano yameendelea nchini Tunisia baada ya maelfu ya raia kujikusanya nje ya jengo la bunge nchini humo na kudai serikali inayoongozwa na chama cha kiislamu cha Enhada kujiuzulu.  

Waandamanaji nchini Tunisia
Waandamanaji nchini Tunisia tunisia-live.net
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa bunge Mustafa Ben Jaafar amesema kuwa Wajumbe waliochaguliwa wamesimamishwa kazi yao mpaka mazungumzo kati ya serikali na upinzani yatakapoanza kujadili kuhusu mashambulizi yaliyosababisha kifo cha mbunge wa upinzani Mohamed Brahimi mnamo tarehe 25 mwezi julai.

Waandamanji hao walionekana kubeba picha za kiongozi aliyeuawa Mohamed Brahimi sambamba na mwanasiasa wa upinzani Chokri Belaid ambaye alishambuliwa kwa risasi na kuuawa mnamo mwezi wa pili.

Kidole cha lawama za Mauaji hayo yote kimeelekezwa kwa chama cha kiislamu Enhada na baraza la mawaziri likikosolewa kushindwa kutawala kwa viwango vilivyotarajiwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.