Pata taarifa kuu
MISRI-MORSI

Rais wa Misri Morsi asisitiza kutong'oka madarakani, waandamanaji waendelea kupiga kambi

Watu 16 wameuawa na kundi la watu wasiojulikana na kuwajeruhi wengine 200 katika shambulio jijini Cairo dhidi ya Watu wanaomuunga mkono Rais wa Misri Mohamed Morsi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limekuja wakati ambapo Kiongozi hiyo wa kiislamu ameapa kuwa hatasikiliza matakwa ya waandamaji wanaomtaka ajiuzulu.
 

Rais Morsi amewaambia Raia wa Misri kuwa alishinda uchaguzi na kuwa ataendelea kutekeleza wajibu wake ingawa kumekuwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu.
 

Hata hivyo pamoja na msimamo wa Morsi bado hakuna dalili za kupatikana kwa maelewano baina ya pande hizo mbili hatua ambayo inamweka Morsi katika wakati mgumu katika mustakabali wa siasa za Misri.
 

Mkuu wa majeshi wa Misri Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, ambaye anaonekana kuwa na nguvu amenuia kusaidia kumalizika kwa mgogoro huo lakini hayuko tayari kuirejesha Misri katika utawala wa kijeshi kama ilivyofanyika mwaka 2011 na 2012.
 

Maandamano yanaendelea kupamba moto licha ya Morsi Kkutoa wito wa kuwepo mazungumzo ili kumaliza tofauti zilizopo kwa manufaa ya Misri na wananchi wake.
Maandamano kama hayo yalimwondoa madarakani Rais wa wakati huo Hosni Mubarak na hali hiyo sasa inaonekana kumgeukia Rais Mohamed Morsi ambaye ameweka ngumu kuondoka madarakani kama waandamanaji wanavyotaka.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.