Pata taarifa kuu
MISRI-CAIRO

Mawaziri wanne wajiuzulu Misri, Upinzani wampa siku moja Morsi Kung'atuka

Mawaziri wanne wa Misri wamejiuzulu nyadhifa zao leo Jumatatu, siku moja baada ya maandamano ya umma kumpinga rais Mohamed Morsi kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini humo. 

Mawaziri wanne wajiuzuru uwaziri nchini Misri
Mawaziri wanne wajiuzuru uwaziri nchini Misri au.news.yahoo.com
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao ni pamoja na waziri wa masuala ya utalii, mazingira, mawasiliano na masuala ya kisheria ambao kwa pamoja wamewasilisha barua zao za kuacha kazi kwa waziri mkuu Hisham Qandil.
Hayo yanajiri wakati upinzani nchini humo umempa rais Morsi siku moja kuondoka madarakani ama kuwa tayari kukabiliana na ukaidi wa raia baada ya maandamano makubwa yaliyomtaka rais huyo wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia kung'atuka madarakani mwaka mmoja tangu achaguliwe.

Wizara ya afya imesema kuwa watu 16 wamepoteza maisha katika maandamano ya nchi nzima, ikiwa ni pamoja na wanane waliouwawa katika mapigano kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi nje ya makao makuu ya chama cha Muslim Brotherhood ambacho anakiongoza ambapo watu wengine watatu wameuwawa katika jimbo la kati la Assiut.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.