Pata taarifa kuu
AU-MISRI-ETHIOPIA

Umoja wa Afrika wataka Misri na Ethiopia kumaliza mzozo wa Mto Nile

Umoja wa Afrika unaitaka Misri na Ethiopia kuketi katika meza ya mazungumzo na kumaliza mzozo kati yao kuhusu hatua ya serikali ya Addis Ababa kubadilisha mkondo wa maji ya Mto Nile kwa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa wa Umoja huo Nkosazana Dlamini-Zuma amesema kuwa mataifa hayo mawili ni lazima yafikie makubaliano ya pamoja  wala sio kuendelea kuzozana kuhusu mmiliki halisi wa Mto huo.

Rais wa Misri Mohammed Morsi amesema kuwa njia zote ziko wazi kujaribu kutatua mvutano huo na  Misri  iko tayari kukabiliana na Ethiopia ikiwa itaendelea na mradi huo kwa kutumia maji ya Mto huo.

Morsi ameongeza kuwa hajatangaza vita lakini serikali yake haitaruhusu mkondo wa maji ya Mto Nile kutumiwa katika mradi huo wa umeme bila la idhini yake.

Misri wamepuuzilia mbali ripoti ya watalaam wa kimataifa kuhusu mradi huo, ripoti inaonesha kuwa  haitakuwa na madhara yoyote kuhusu maji ya Mto huo.

Mwezi uliopita, Ethiopia ilianza kuelekeza maji ya Mto Nile upande wao ili kufanikisha mradi huo wa umeme wenye Megawatts 6,000 na itaigharimu Dola Bilioni 4 nukta 7 .

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa hayo mawili wanatarajiwa kukutana jijini Addis Ababa siku chache zijazo kujaribu kutafuta suluhu la mzozo huu ambao huenda ukasababisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Addis Ababa na Cairo.

Misri inasema ni lazima mkataba wa kihistoria wa Mto huo unaoipa mamlaka ya kuwa na usemi mkubwa kuhusu maji ya Mto huo uliofikiwa mwaka 1929 na 1959  uheshimiwa na inaishtumu Ethiopia kwa  kutowaomba ruhusu kabla ya kuanza mradi huo.

Ethiopia kwa upande wake inasema ilishauriana kikamilifu  na serikali ya Misri kabla ya kuanza kwa mradi huo ,suala ambalo Misri inakanusha.

Mwaka 2010 mataifa ambayo Mto huo wa Nile unapitia walitia sahihi makubaliano ya kuruhusu mataifa wanachama kufanya miradi kutumia maji ya Mto huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.