Pata taarifa kuu
MISRI-ETHIOPIA

Misri yasema haijatangaza vita dhidi ya Ethiopia kutokana na mzozo wa Mto Nile

Misri inasema njia zote ziko wazi kujaribu kutatua mvutano kati yake na Ethiopia kuhusu mradi wa serikali ya Addis Ababa kujenga bwawa la kuzalisha umeme kutumia maji ya Mto Nile.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mohammed Morsi hata hivyo anasema serikali yake iko tayari kukabiliana na Ethiopia ikiwa itaendelea na mradi huo kwa kutumia maji yake.

Morsi ameongeza kuwa hajatangaza vita lakini serikali yake haitaruhusu maji ya Mto Nile kutumiwa kwa mradi huo wa umeme bila la idhini yake.

Tayari Ethiopia imeshaanza kuelekeza mkondo wa Mto Nile ili kufanikisha mradi huo wa umeme wenye Megawatts 6,000 na itaigharimu Dola Bilioni 4 nukta 7.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa hayo mawili wanatarajiwa kukutana jijini Addis Ababa siku chache zijazo kujaribu kutafuta suluhu la mzozo huu ambao huenda ukasababisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Addis Ababa na Cairo.

Misri inasema ni lazima mkataba wa kihistoria wa Mto huo unaoipa mamlaka ya kuwa na usemi mkubwa kuhusu maji ya Mto huo uliofikiwa mwaka 1929 na 1959  uheshimiwa.

Mwaka 2010 mataifa ambayo Mto huo wa Nile unapitia walitia sahihi makubaliano ya kuruhusu mataifa wanachama kufanya miradi kutumia maji ya Mto huo.

Wakili Ojwang Agina ni mchambuzi wa siasa za kimataifa anasema kuwa suluhu pekee la mzozo huu ni mazungumzo kati ya serikali ya Ethiopia na Misri.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.