Pata taarifa kuu
NIGERIA

Watuhumiwa 65 wa Boko Haram watiwa mbaroni

Jeshi nchini Nigeria limewatia mbaroni watuhuniwa 65 wa kundi la Boko Haram na kutaifisha simu za mkononi na magari iki wa ni hatua ya kuendelea na operesheni yao ya kuwasaka wapiganaji wa kundi hilo la kiislamu kwenye mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno. 

Wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika operesheni dhidi ya Boko Haram
Wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika operesheni dhidi ya Boko Haram channelstv.com
Matangazo ya kibiashara

Jeshi nchini humo limetoa amri ya kutotembea kwa saa ishirini na nne kwenye miji yote mitatu ambayo rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari, ambapo mipaka na njia kuu za kibiashara zimefungwa kuwadhibiti wapiganaji wa Boko Haram.

Lakini wakati hali ya kutotembea hovyo kwa saa 24 ikitangazwa, baadhi ya wananchi na wabunge wameonesha hofu ya kuzuka machafuko zaidi kwa kuwa waumini wengi wa kiislamu wanashindwa kwenda msikitini.

Jana Jumapili jeshi la nchi hiyo lilifunga barabara na njia zinazotumika kibiashara ambazo zinaingia kwenye mji muhimu ambako wapiganaji wa kundi la Boko haramu wanadaiwa kujificha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.