Pata taarifa kuu
SOMALIA

Oparesheni kubwa ya kusaka vilipuzi na silaha yazinduliwa mjini Mogadishu

Maafisa wa usalama nchini Somalia wanafanya Oparesheni kubwa mjini Mogadishu kuwasaka vilipuzi na silaha zilizotumiwa kutekeleza shambulizi la kujitoa mhanga siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanayakagua  magari yote yanayoingia katikati ya mji katika Opareshi ambayo wakaazi wa Mogadishu wanasema si ya kawaida.

Ali Ismail mmoja wa wakaazi wa mji huo wanasema kuwa mbali na polisi hao kuyachunguza magari yote wanawakamata watu wanaokwenda katikati ya mji.

Watu 34 waliuawa mjini Mogadishu Jumapili iliyopita baada ya watu kadhaa kutekeleza shambulizi la kujitoa mhanga ndani ya Mahakama moja mjini humo.

Kundi la kigaidi la Al-Shabab linaloshirikiana na Al –Qaeda limekiri kutekeleza mashambulizi hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa mjini humo katika siku za hivi karibuni.

Maafisa wa usalama mjini Mogadishu wanasema kuwa zaidi ya watu 50 wamejeruhiwa huku Waziri wa mambo ya ndani Abdikarin Hussein Guled akisema maafisa wa usalama wa serikali sasa wamethibiti hali hiyo na shughuli katika mji huo zimerejea kama kawaida.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga ambaye juma lililopita alinukuliwa akisema kuwa kundi la Al-Shabab limesambaratika na wanajeshi wa Umoja wa Afrika wamewafukuza mjini Mogadishu, amesema ameshangazwa na mashambulizi  hayo.

Mahiga ameelani mashambuzli hayo na kuongeza kuwa visa vya kigaidi kama hivyo havitakwamisha juhudi za kuijenga upya nchi ya Somalia na kupata usalama na uongozi thabiti.

Wachambuzi wa siasa na usalama wanasema kuwa shambulizi hili linaonesha kuwa bado usalama haujaimarika nchini Somalia hasa mjini Mogadidhu.

Francis Onditi ni mtalaam wa usalama akiwa jijini Nairobi nchini Kenya ameiambia RFI Kiswahili Jumatatu asubuhi kuwa mashambulizi haya ya mwisho wa juma yanadhihirisha kuwa bado wanamgabo hao wa Al-Shabab wanajificha mjini Mogadishu na viunga vyake.

Wanajeshi ya wa Umoja wa Afrika zaidi ya elfu saba wanapambana na wanagambao wa Al-Shabab nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.