Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Ufaransa yaahidi kuendelea kuisaidia Mali kukabiliana na makundi ya wapiganaji

Ufaransa imeihakikishia Mali kuwa itaendelea kuunga mkono jitihada za kijeshi katika kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

REUTERS/John Vizcaino
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Bamako kujadili mpango wa majeshi ya Ufaransa kuondoka nchini humo, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema wamewasilisha pendekezo kwa Umoja wa Mataifa UN la kutoa msaada wa wanajeshi elfu moja katika kuendeleza jitihada za kukabiliana na vitendo vya ugaidi.

Aidha, Fabius amesisitiza kuwa mazungumzo ya kidemokrasia ni muhimu pia katika utafutaji wa suluhu ya mzozo katika nchi hiyo.

Mapema mwaka huu Ufaransa ilipeleka wanajeshi wake elfu nne nchini Mali kupambana na wapiganaji wa kiislamu na kuwasambaratisha kwenye ngome zao muhimu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.