Pata taarifa kuu
SOMALIA-ETHIOPIA-AMISOM

Wanajeshi wa Ethiopia waanza kuondoka Kusini mwa Somalia

Vikosi vya Umoja wa Afrika AMISOM vilivyoko nchini Somalia vinajiandaa kushika doria kwenye maeneo ambayo wanajeshi wa Ethiopia wameanza kuondoka.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa majeshi ya Ethiopia yaliyoko nchini humo amethibitisha kuondoka kwa wanajeshi wake kwenye mji wa Hudur ulioko jimboni Bokool siku ya jumapili ambapo punde mara baada ya kuondoka kuliripotiwa wanamgambo wa Al-Shabab kurejea katika eneo hilo.

Mkuu wa majeshi ya AMISOM nchini Somalia Andrew Gutti amesema licha ya kuondoka kwa vikosi vya Ethiopia vilivyokuwa nchini humo tangu mwezi Novemba mwaka 2011 havitaathiri hali ya usalama nchini humo licha ya kuwepo wasiwasi.

Hofu ya kiusalama imetanda nchini Somalia kufuatia kuanza kuondoka kwa vikosi vya Ethiopia ambavyo kwa sehemu kubwa vilifanikisha kuwadhibiti wanamgambo wa Al-Shabab.

Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema kuwa ikiwa wanajeshi wa Ethiopia wataondoka Kusini mwa Somalia basi wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM wapatao 17,000 watalazimika kusambaa zaidi Kusini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Kenya ambao walijumuishwa ndani ya wanajeshi wa AMISOM wameendelea kushika doria Kusini mwa nchi hiyo kupambana na Al -Shabab na wamefanikiwa kuchukua uthibiti wa miji kadhaa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.