Pata taarifa kuu
Tunisia-Maandamano

Wanachama wa chama tawala cha Tunisia waandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo

Wanachama wa chama kikuu cha kiislamu nchini Tunisia ambacho ndio chama tawala cha Enhada wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis jumamosi hii ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya polisi kukabiliana na waombolezaji katika mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya jumatano.

REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa Enhada maandamano ya hayo yanalenga kutetea uhalali wa bunge la nchi hiyo ambalo limetawaliwa na idadi kubwa ya wanachama wa chama hicho.

Aidha maandamano hayo yanalenga kupinga harakati za wapinzani zinazoendelea hivi sasa ambao wanakituhumu chama tawala kwa kuhusika na mauaji ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid.

Tukio la kuuawa kwa kiongozi huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa kwa serikali limeliingiza Taifa hilo katika ukurasa mwingine wa ghasia wakati chama tawala nacho kikizidi kugawanyika baada ya waziri mkuu Hamadi Jebali kuwa katika mkakati wa kuunda serikali mpya ya wataalamu.

Chama cha kutetea haki za binadamu cha nchini Tunisia kimesema hali hiyo inaendelea kushuhudiwa nchini humo kutokana na chama tawala kushika nyadhifa nyingi zaidi ndani ya serikali huku kikitoa wito kwa wanasiasa kulindwa ili kuepukana na vitisho wanavyokumbana navyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.