Pata taarifa kuu
Algeria

Hofu yatanda nchini Algeria kufuatia vifo na kutekwa nyara kwa Raia wa kigeni

Hofu imeendelea kutanda juu ya usalama wa Mateka wa maataifa ya kugeni waliotekwa na wanamgambo wa Kiislamu nchini Algeria wakiwa Wafanyakazi katika Kiwanda cha Gesi huku mataifa hayo yakihaha kuwanusuru na kifo.

Barabara inayoelekeza njia ya Menas Kiwanda cha Gesi kilipo
Barabara inayoelekeza njia ya Menas Kiwanda cha Gesi kilipo Reuters/Kjetil Alsvik/Statoil/Handout
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo hao wameendelea kuwashikilia Wafanyakazi hao huku Wanajeshi wa Algeria wakiwa wamekizingir kiwanda hicho kinachopatikana mjini Amenas na kumilikiwa na Shirika la BP.

Waziri wa habari wa Algeria, Mohamed Said ameonesha Masikitiko yake na yale yaliyotokea na kuthibitisha kuwa Operesheni ya kijeshi ya kuwaokoa mateka hao inaendelea vizuri.

Wanamgambo wa kiislamu wakiwa wamejihami barabara kwa silaha nzito walivamia Kiwanda cha gesi na kuwaua Wafanyakazi wawili Raia wa Uingereza wakionesha kutofurahishwa na Ufaransa kupeleka Vikosi vyake nchini Mali.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.