Pata taarifa kuu
MALI

Uwepo wa wanamgambo wa kiislamu Kaskazini mwa Mali waathiri uchumi na biashara

Wanamgambo wa kiislamu wanaoshikilia eneo la Kaskazini mwa nchi ya Mali wanadaiwa kuzorotesha hali ya uchumi katika mji wa Bamako ambako wageni wameanza kuondoka huku uhaba wa ajira na kupanda kwa bei za bidhaa vikiongezeka. 

Waasi wa kiislam Kaskazini mwa Mali
Waasi wa kiislam Kaskazini mwa Mali english.alarabiya.ne
Matangazo ya kibiashara

Taasisi ya fedha duniani IMF baada ya kuzuru nchi hiyo mwezi uliopita imeeleza kuwa uchumi wa Mali kwa sasa unapita katika kipindi kigumu kutokana na mavuno duni katika msimu wa mwaka 2011-2012 sambamba na mapinduzi yaliyofanywa mwezi Machi.

Wanamgambo wa kiislamu wanashikilia eneo kubwa la Kaskazini mwa Mali tangu kupinduliwa madarakani kwa rais wa zamani wa taifa hilo Amadou Toumani Toure mnamo mwezi Machi mwaka 2012.

Kufuatia mapinduzi hayo na eneo hilo kukaliwa na wanamgambo hao uzalishaji wa mazao ya kilimo na mahusiano ya kibiashara vimeathirika huku hali ya usalama mdogo ukichochea kwa kiasi kikubwa kushuka kwa ziara nchini Mali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.