Pata taarifa kuu
KENYA

Raila Odinga kupeperusha bendera ya Muungano wa CORD katika kinyang'anyiro cha Urais wa Kenya

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameidhinishwa rasmi kuuwakilisha muungano wa CORD katika kuwania nafasi ya Urais wa nchi hiyo na atachuana vikali na Makamu wake Uhuru Kenyatta ambaye anatarajiwa kuuwakilisha muungano wa jubilee.

Photo : Khaled Desouki /AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombe wengine wa muungano wa CORD walioidhinishwa jana ni pamoja na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka ambaye atakuwa mgombea mwenza wa kiti cha Urais pamoja na Mozes Wetangula ambaye atasimamia maswala ya bunge.

Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta ambaye alijiuzulu wadhifa wa Uwaziri wa fedha mwezi january mwaka huu baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kumuona ana kosa la kujibu kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 atatambulishwa rasmi leo jumapili kama mgombea urais wa muungano wa jubilee katika sherehe zitakazofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi.

Takribani wapiga kura milioni 14 wamejisajili katika zoezi lililoendeshwa na tume ya uchaguzi nchini humo IEBC na raia wa Taifa hilo wamekuwa wakionywa kuepuka mikasa ambayo inaweza kuliingiza tena taifa hili katika machafuko kama yale yaliyozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.