Pata taarifa kuu
DRCongo

Waasi watoa masharti ya kuondoka Goma, wataka Etienne Tshisekedi aondolewe kizuizi

Waasi wa kundi la waasi wa M23 wamesema wako tayari kuomdoka katika mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wiki moja baada ya kuushikilia baada ya majeshi ya Serikali kukimbia mapambano katika na kuwaacha waasi hao wakiuteka na kuuweka katika himaya yao.

AFP PHOTO / Junior D.Kannah
Matangazo ya kibiashara

Kamanda mwandamizi wa kundi hilo Kanali Antoine Manzi amesema kuwa wapiganaji wake wako tayari kuondoka Goma ili kupisha mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro unaondelea mashariki mwa DRC.

Hata kundi la M23 limesema kuwa litaondoka tu mjini Goma serikali ya Joseph Kabila itatekeleza mahitaji yao ingawaje hapo awali ilitangazwa kuwa wangeondoka katika mji huo.

Katika masharti yao waasi hao wa M23 wanaitaka serikali ya DRC kuivunja Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kabla ya kuamua kuondoka mjini Goma ambako kumekuwa na hali ya wasiwasi huku raia wakikimbia makazi yao.

Katika hatua nyingine waasi hao wameitaka serikali ya Kabila kumwachia mwanasiasa maarufu na kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi kutoka katika kizuizi cha nyumbani kwake.

Kiongozi wa siasa wa kundi la M23 Jean-Marie Runiga amesema kuwa kama masharti hayo yatatekelezwa wao wataondoka Goma mara moja na kuanza mazungumzo ya kusaka suluhu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.