Pata taarifa kuu
Cote d'Ivoire

Rais Allassane Outtara avunja baraza la mawaziri Cote d'Ivoire baada ya vyama kutofautiana bungeni

Rais wa Cote d'Ivoire Allassane Outtara ametangaza kulivunja baraza lake la mawaziri ambalo aliliunda mwezi March mara baada ya kumalizikka kwa machafuko ya mara baada ya uchaguzi mkuu.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu Amadou Gon Coulibaly amethibitisha rais Outtara kulivunja baraza lake la mawaziri linaloongozwa na waziri mkuu Jeannot Kouadio Ahoussou mara baada ya viongozi wa vyama vya RDR cha rais Ouattara na vile vya PDCI na UDPCI kutofautiana bungeni.

Ikulu imesema kuwa tayari rais amewasiliana na viongozi wengine wa vyama vinavyounda serikali na wameunga mkono mabadiliko ya serikali.

Rais huyo amefanya mabadiliko hayo akilenga kuleta mabadiliko ya kuijenga upya Cote d'Ivoire ambayo ilikabiliwa na kipindi cha machafuko baada ya uchaguzi katika kipindi cha 2010 na 2011.

Katika Serikali inayoondoka baada ya kuvunjwa Ouattara alijipa madaraka ya wizara ya ulinzi akiwa na lengo la kulifanyia mabadiliko na kuliboresha jeshi katika harakati za kukabiliana na mgogoro ulioibuka baada ya uchaguzi huo.

Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo alikataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi na Ouattara kutangazwa mshindi.

Katika mgogoro huo watu wasiopungua 3,000 waliuawa kabla ya Gbagbo kukamatwa na sasa anasubiri hatma ya kesi yake ya makosa ya uhalifu dhidi binadamu katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC huko The Hague nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.