Pata taarifa kuu
NIGERIA

Wabunge Nigeria wapitisha muswada unaopinga haki za mashoga

Wabunge nchini Nigeria wamepitisha muswada unaopinga vikali haki za mashoga ikiwemo kupiga marufuku ndoa za jinsi moja na kupiga marufuku matangazo au maonesho yanayowahamasisha wapenzi wa jinsia moja.

Reuters/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Muswada huu ambao ulipitishwa na maseneta ulipelekwa bungeni na kupigiwa kura na muswada huu utapitiwa kifungu hadi kifungu.

Wabunge nchini humo wamesema kuwa muswada huu umepita ukiungwa mkono na wabunge wengi kwa kuwa maswala ya ndoa za jinsia moja ni kinyume cha sheria na maadili.

Muswada huu pia umepiga marufuku vyama vya mashoga, hali iliyozua maswali juu ya uwezekano wa hatua hii kuathiri misaada ya dawa za ARV kupitia kwenye jumuia hizi kutoka nje.

Muswada huo umepitishwa kwa sababu unaenda kinyume na maadili ya dini na tamaduni za kiafrika na ndoa za mashoga haziwezi kupewa nafasi katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Mwaka 2014 bunge la seneti la Nigeria lilipitisha muswada ungewezesha watu wenye ndoa za jinsi moja kupatiwa kifungo cha mpaka miaka 14 na miaka 10 kwa mtu yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.