Pata taarifa kuu
MALI

Burkina Faso yashinikiza mazungumzo ya kurejesha amani Mali

Mazungumzo yenye lengo la kuyahamasisha makundi yenye kumiliki silaha huko kaskazini mwa Mali yamepigwa jeki na serikali ya Burkina Faso tangu Jumapili novemba 4 mjini Ouagadougou ambapo kwa mara ya kwanza ujumbe wa wapiganaji wa Ansar Dine umeshiriki.

Wanajeshi wa serikali ya Mali wakijadili namna ya kupambana na waasi wa nchi hiyo
Wanajeshi wa serikali ya Mali wakijadili namna ya kupambana na waasi wa nchi hiyo REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wajumbe wa kundi hilo la waasi linaloongozwa na Alghabass Ag Intalla mbunge wa kaskazini mwa nchi hiyo akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Burkina faso limejiondoa na kuonesha kutokuwa tayari kuendelea kushiriki katika mchakato wa kurejesha amani huko Mali.

Lengo la mkutano huo ni kuyataka makundi yote kuachana na suala la uungwaji mkono kutoka makundi ya kigaidi kaskazini mwa Mali.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa suala muhimu kwa sasa ni kujua waasi hao wanafadhiliwa na nani.

Mataifa katika ukanda wa Afrika magharibi sambamba na jumuiya ya kimataifa yanahofu huenda eneo la kaskazini mwa Mali likawa kitovu kipya cha ugaidi.

Juma lililopita Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alihimiza umoja wa nchi za magharibi ECOWAS uchukue hatua dhidi ya Al-Qaeda, usafirishaji wa dawa za kulevya, utekaji nyara na makosa mengine ya kihalifu yanaoigeuza Mali kuwa sehemu ya magaidi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.