Pata taarifa kuu
NIGERIA

Serikali ya Nigeria yatangaza utayari wake wa kuzungumza na Kundi la Boko Haram

Serikali ya Nigeria imetangaza utayari wake kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Kundi la Boko Haram ili kupata suluhu ya mashambulizi ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kundi hilo tanfu mwaka 2009.

Mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Kundi la Boko Haram nchini nigeria na kuleta madhara
Mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Kundi la Boko Haram nchini nigeria na kuleta madhara Reuters/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Rais Goodluck Jonathan, Reuben Abati ndiye amethibitisha utayari wa serikali ya Nigeria kuwa tayari kutumia njia ya mazungumzo ili kumaliza mashambulizi ambayo yamekuwa yakitekelezwa na Boko Haram.

Kauli ya Serikali imekuja baada ya kufanyika Mkutano wa Waandishi wa Habari ulioendeshwa kwa njia ya Televisheni na kuongozwa na Mtu ambaye amejitaja kuwa Kiongozi wa Boko Haram Abu Mohammed Ibn Abdulaziz.

Abdulaziz amefanya mkutano huo na waandishi wa habari Kaskazini Mashariki mwa Jiji la maiduguri na kueleza wao wapo tayari kuzungumza na serikali ili kueleza kile ambacho wanakihitaji.

Kiongozi huyo wa Boko Haram amekiri nafasi ya mazungumzo ipo wazi ili wao waweze kusalisha madai yao ya msingi lakini kwenye maelezo yake ameshindwa kueleza kama wanataka uwepo wa Shria za Kiislam.

Abdulaziz amependekeza mazungumzo hayo yafanyike nchini Saudi Arabia na kuratibiwa na Kiongozi wa zamani wa Jeshi nchini Nigeria Muhammadu Buhari ambaye alianguka kwenye uchaguzi wa Rais mwaka 2011 alipopambana na Rais Jonathan.

Hakuweza kubaini mara moja kama Abdulaziz amechukua nafasi ya Abubakar Shekau ambaye amekuwa akiongoza Kundi la Boko Haram na kutajwa kama miongoni mwa magaidi wanaosakwa na Marekani.

Msemaji wa Rais Jonathan, Abati amekiri kuona mkutano huo na yeye kusema serikali yake ipo tayari kuketi mezani na Boko Haram ili kuzungumza nao na kuelewa madai ya msingi ambayo wanayahitaji.

Abati ameongeza kwa muda mrefu Rais Jonathan alishatoa wito kwa Viongozi wa Kundi la Boko Haram kujitoka ili wafanye mazungumzo ambayo yamekuwa suluhu ya kumalizwa kwa mashambulizi ambayo yanaendelea kufanywa.

Machafuko ambayo yamekuwa yakipamngwa na kutekelezwa na kundi la Boko Haram tangu mwaka 2009 yamesababisha vifo vya watu elfu mbili mia nane wakiwemo raia na askari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.