Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Kiongozi wa Upinzani nchini Mauritania ataka Jeshi lijiweke kando na siasa

Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Mauritania Khadiata Malik Diallo ametoa wito kwa Jeshi nchini humo kujiweka kando na masuala ya siasa na badala yake jukumu hilo lifanywe na Vyama vya Siasa pekee.

Rais wa Mauritania Mohamed Abdel Aziz ambaye yupo nchini Ufaransa akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake
Rais wa Mauritania Mohamed Abdel Aziz ambaye yupo nchini Ufaransa akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake REUTERS/Darrin Zammit Lupi/Files
Matangazo ya kibiashara

Diallo ametoa kauli hiyo kutokana na kile ambacho amekieleza kwa kipindi cha miaka zaidi ya arobaini wanajeshi wameendelea kushika utawala wa nchi hiyo kitu kinachotoa tafsiri Mkuu wa Majeshi ndiye mwenye nguvu.

Makamu wa Rais huyo wa Chama Cha UFP Diallo amesema hawataki kuona Jeshi likiingia shughuli za siasa kuazia sasa na badala yake wanataka yule ambaye anashiriki siasa aachane na kazi ya Jeshi.

Kauli ya Diallo imekuja kutokana na uwepo wa minong'ono ya Jeshi huenda likachukua Utawala nchini Mauritania kutokana na sasa Rais Mohamed Ould Abdel Aziz kuwa nje ya taifa hilo akipatiwa matibabu.

Rais Abdel Aziz alipigwa risasi na mmoja wa walinzi wake kwa bahati mbaya na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu nchini Ufaransa huku duru za kiserikali zikisema afya yake inaendelea vyema.

Wafuasi wa Upinzani nchini Mauritania wamefanya maandamano makubwa katika Jiji la Nouakchott wakitaka kuwepo na uwazi wa taarifa kuhusiana na hali ya afya ya Rais Abdel Aziz ambaye yupo Paris.

Taarifa kutoka nchini Mauritania zinaeleza Rais Abdel Aziz amesha ruhusiwa kutopka Hospital tangu juma lililopita lakini ameendelea kusalia nchini Ufaransa bila ya kuelezwa sababu zilizochangia hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.