Pata taarifa kuu
MALI

Nchi wanachama za ECOWAS zinaendelea kujadili uwezekano wa kupeleka Jeshi nchini Mali kukabiliana na waasi

Mawaziri wa Ulinzi na wale wa Mambo ya Nje na Ushirikiano kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wakijadi uwezekano wa kupelekwa kwa Jeshi nchini Mali ili kukabiliana na makundi ya uasi ambayo yanapambana na serikali Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wapiganaji wa Makundi ya Waislam wenye msimamo mkali Kaskazini mwa Mali wanaopambana na serikali
Wapiganaji wa Makundi ya Waislam wenye msimamo mkali Kaskazini mwa Mali wanaopambana na serikali REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao wamejadiliana kwa kina namna ya kushughulikia mgogoro wa kisiasa nchini Mali ambao umesababisha kugawanyika kwa Taifa hilo katika sehemu mbili moja ikiwa chini ya serikali wakati ile nyingine ikiwa chini ya utawala wa Waasi hasa eneo la Kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cote D'Ivoire Daniel Kablan Duncan baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kusema wanamatumaini ya kuweza kufikia makubaliano ya kupelekwa kwa jeshi nchini humo licha ya kuendelea kukabiliana na upinzani kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Mkutano wa ECOWAS ni matokeo ya ombi lililowasilishwa mapema mwezi huu na Rais wa Serikali ya Mpito ya Mali Dioncounda Traore ambaye anataka usaidizi wa kijeshi ili kukabiliana na waasi wanaodhoofisha serikali yake.

Mkuu wa Tume ya ECOWAS Kadre Desire Ouedraogo ameongeza kuwa licha ya wao kuwa tayari kuweza kutoa jeshi kwa Mali lakini watahakikisha hatua za kijeshi zinachukuliwa kwa wale waliotenda makosa ya uhalifu.

Balozi wa Cote D'Ivoire katika Umoja wa Mataifa UN Youssoufou Bamba ameliambia Baraza la Usalama nchi za Afrika za Magharibi zinahitaji ndege za kijeshi kwa lengo la kufanya uvamizi wa kijeshi huko Mali.

Licha ya jeshi hilo kuonekana linahitaji nchini Mali lakini Senegal na Ghana zimesema msimamo wake ni kutoshiriki kwenye jeshi hilo lakini msuluhishi mkuu wa mgogoro huo ni Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore.

Mkuu wa Tume ya Kutetea Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay alilaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unaendelea kufanyika Kaskazini mwa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.