Pata taarifa kuu
Mali-mauaji

Serikali ya Mali yaanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya wahubiri 16 wa kiislam

Serikali nchini Mali imeamuru kuanzisha uchunguzi dhidi ya mashambulizi yaliotokea jana jumapili ambapo watu kumi na sita wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kiislam waliuawa na jeshi la Mali wakiwemo watu wanane raia wa Mali na wengine wanane wa Mauritania. Serikali ya Mauritania imelaani mauaji hayo.

Jeshi la Mali katika doria
Jeshi la Mali katika doria © Serge Daniel/RFI
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Mali ambalo halikupoteza mwanajeshi wake hata mmoja lilifyatulia risase gari lililokuwa limewabeba wahubiri wa kiislam  wanao sadikiwa kuwa wafuasi wa kundi la kiislam ambao walikataa kusimama kwa ajili ya uchunguzi katika eneo la Diabali kwenye umbali wa kilometa 175 kaskazini mwa mji wa Segou, duru mbalimbali zimethibitisha.

Mji wa Segou upo kwenye umbali wa kilometa 235 ya mji wa Bamako kaskazini mashariki mwa emeo la kaskazini linalo kaliwa tangu kipindi kadhaa na makundi mbalimbali ya kiislam likiwemo kundi la Ansar Dine na kundi la Mujao linalofungamana na mtandao wa Alqaeda la (AQMI)

Duru za kijeshi na kiusalama zaarifu kuwa mashambulizi hayo yalitokea baada ya waislam hao kukataa kusimama, wakati walipotakiwa kusimama, na baadae jeshi likawachukulia kama aduwi na ndipo kuwashambuliwa.

katika taarifa iliotolewa na serikali jana jumalipi, watu wanane raia wa Mali na wengine wanane raia wa Mauritania wameuawa na kutangaza kuanzisha uchunguzi na baadae kutowa ripoti nchini Mali na Mauritania.

Taarifa hiyo imesema kwamba serikali ya Mali imesikitishwa na tukio hilona imemtuma mjumbe wake jijini nouakchott ambae ni waziri wa mambo ya nje Tieman Coulibaly kupeleka salam za rambi rambi kwa serikali ya Mauritania.

Jana jioni shirika la habari la Mauritania limetasngaza kwamba wahubiri kumi na wawili wa dini ya kiislam waliokuwa katika harakati zao za kuhubiri wameuawa na vyombo vya habari nchini Mali.

Viongozi wa Mauritania, wanashirikiana na uongozi wa Mali ili kupata taafira zaidi na kusafirisha miili ya raia wake kwa ajili ya shughuli za mazishi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.