Pata taarifa kuu
MALI-mauritania

Kiongozi wa kundi la AQMI katika ukanda wa Sahel apoteza maisha katika ajali ya barabarani

Kiongozi wa mtandao wa Alqaeda katika maeneo ya jangwa la Sahel Nabil Abou Alqama ameuawa kutokana na ajali ya gari iliotokea jana jumapili septemba 9, 2012 katika maeneo ya kaskazini mwa Mali takriban kilometa 200 na mji wa Gao akiwa njiani kuelekea katika mkutano ulio yakusanyisha makundi mbalimbali ya kiislam katika ukanda wa Sahel.

Wapiganani wa makundi ya kislam yenye mafungamano na kundi la Aqmi
Wapiganani wa makundi ya kislam yenye mafungamano na kundi la Aqmi AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Jina lake halisi ni Nabil Makhloufi ambae alijulikana sana kwa jina la Nabil Abou Alqama alipenda kufia kwenye uwanja wa mapambano, lakini mwishowe ameuawa kwa ajali ya gari.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ajali hiyo imetokea kati ya mji wa Gossi na Gao wakati gari lake lililopokuwa likitokea timbuktu. Habari zaidi zaarifu kuwa kiongozi huyo alikuwa akielekea kwenye mkutano wa makundi ya kiislam katika eneo hilo.

Nabil Abou Alqama mwenye umri wa miaka 35, alikuwa mwanajeshi zamani katika jeshi la Algeria kabla ya kujiunga na kundi la Islamic Group Army (IGA) na baadae kujiunga na kundi la Salafist Group for Preaching and Combat (SGPC) na haitmae kulekea kaskazini mwa Mali.

Mwaka uliopita Amir wa kundi la Alqaeda katika maghreb ya kiislam Abdelmalek Droukdel alimteuwa Nabil kuwa kiongozi wa kanda ya 9 ya ukanda wa Sahel ili kusuluhisha mizozo zmbayo imekuwa ikiibuka kati ya makundi mbalimbali katika ukanda huo kutokana na kuwania mara nyingi fidia inayopatikana kwa njia ya dhamana baada ya kuwaachia huru mateka wa nchi za Magharibi

Tangu uteuzi wake, hali katika manaeneo ya Sahel imekuwa ya kutatanisha. Eneo la kaskazini mwa Mali sasa lipo chini ya udhibiti wa makundi yanayopigana jihadi yanayo julikana kuwa na uhusiano na kundi la AQMI. Kwa sasa kinacho salia kujuwa ni ipi hatma ya eneo hilo bada ya kifo cha kiongozi huyo na mateka waliokuwa chini ya usimamizi wa kundi la AQMI.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.