Pata taarifa kuu
Mali

Kundi la kiislam lenye msimamo mkali MUJAO laripoti kumuua mwanadiplomasia wa Algeria

Kundi la kiislam linalodhibiti Eneo la Kaskazini mwa Mali limesema kuwa limemuua mwanadiplomasia wa Algeria aliyekuwa ametekwa nyara Miezi mitano uliyopita baada ya muda wa mwisho uliotolewa kwa Serikali yake kutimiza matakwa yao kukamilika.

Wanamgambo wa MUJAO wakiwa katika Doria nchini Mali
Wanamgambo wa MUJAO wakiwa katika Doria nchini Mali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kundi la MUJAO limesema kuwa Balozi mdogo wa Algeria Tahar Touati aliuawa Jumamosi asubuhi, na kutishia kuwaua mateka wengine watatu walio mikononi mwao ikiwa Algeria haitaridhia madai yao.
 

Kundi la MUJAO liliipa muda Algeria tangu tarehe 24 mwezi Augusti ikiitaka nchi hiyo kuwaacha huru wafuasi wake watatu waliokamatwa kusini mwa nchi hiyo .
 

Mamlaka nchini Algeria imesema kuwa inafanyia uhakiki Ripoti ya kuuawa kwa Mwanadiplomasia huyo Ripoti iliyotolewa katika mtandao wa kundi la MUJAO nchini Algeria na Mauritania.
 

MUJAO ni kikundi kilichoanza harakati zake mwaka 2011, likieleza kuwa kundi lilijiengua kutoka kundi la Al Qaeda la AQIM.
 

Kundi hilo sambamba na Tuareg na Ansar Dine yamedhibiti sehemu kubwa ya Mali baada ya kutokea mapinduzi ya Bamako yaliyofanyika Tarehe 22 mwezi March.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.