Pata taarifa kuu
Afrika Kusini-Zimbabwe

Rais Zuma atakiwa kujiuzulu, Marekani yakemea uvamizi wa ofisi za wanaotetea ushoga nchini Zimbabwe

Ibada maalumu ya mazishi ya wafanyakazi 44 wa mgodi wa Platinum waliouawa na polisi nchini Afrika kusini imefanyika hapo jana huku serikali ya rais jackob Zuma ikiahidi kupata ukweli wa mauaji hayo. 

REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Rais Zuma hakuhudhuria ibada hiyo ingawa alituma wawakilishi wake na kuahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio huku baadhi ya wananchi wakionesha kuchukizwa kwa rais kushindwa kufika wakati wa mazishi hayo.

Julius Malema aliyesimamaishwa uanachama wa chama cha ANC ameshutumu serikali kwa kutekeleza mauji hayo na kumtaka rais Zuma kuwajibika kwa kujiuzulu.
Wakati huohuo Serikali ya Marekani imelaani vikali tukio la uvamizi wa ofisi za

Wakati huohuo wanaharakati wanaotetea ushoga nchini Zimbabwe na kuongeza kuwa tukio hilo ni kinyume na sheria za haki za binadamu na niudhalilishaji.

Jumatatu ya wiki hii polisi nchini humo walivamia ofisi za wanaharakati hao na kuchukua kopyuta pamoja na nyaraka nyingine muhimu katika tukio ambalo watu kadhaa walijeruhiwa.

Polisi nchini Zimbabwe inawashikilia watu 44 ambao wanajihusisha na ndoa za jinsia moja kwa tuhuma ya kwamba wanashikilia nyaraka za siri ambazo zinahatarisha usalama wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.