Pata taarifa kuu
MALI-NIGERIA

Rais wa Nigeria ataka ECOWAS ipeleke jeshi nchini Mali

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema kuwa majeshi ya ECOWAS yatalazimika kuingia nchini Mali kaskazini mwa nchi hiyo endapo mazungumzo kati ya waasi na Serikali yatashindikana.Rais Jonathan amesema kuwa njia ya mazungumzo ni jambo la kwanza kwao lakini iwapo mazungumzo ya kidiplomasia yatashindikana kati ya waasi wa kaskazini mwa Mali na Serikali, watalazimika kuingilia kijeshi. 

, à Lagos, le 4 juin 2012.
, à Lagos, le 4 juin 2012. REUTERS/Akintunde Akinleye
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ameyasema hayo akiwa ziarani nchini Senegal ambako anakutana na rais Macky Sall kuzungumzia mgogoro wa Mali.

Ili majeshi ya ECOWAS yaweze kuingia nchini Mali yatalazimika kupata kibali toka Umoja wa Mataifa.

Wakati huohuo kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Gabon Andre Mba Obame amesisitiza kauli yake ya kutoogopa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuhusu tishio la yeye kukamatwa na kufunguliwa mashataka ya kuandaa maandamano yaliyopigwa marufuku.

Jumatatu ya wiki hii ofisi ya mwendesha mashtaka nchini humo ilitangaza kuwa ingetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo kufuatia matamshi yake ya kuhatarisha usalama kwa kutishia maandamano zaidi nchini humo.

Wafuasi wa Obame wamekuwa wakifanya maandamano kwenye mji wa Lbriville kuendelea kupinga ushindi wa rais Ali Bongo Ondimba ambao wao wanadai upinzani ulishinda uchaguzi wa mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.