Pata taarifa kuu
TANZANIA-MALAWI

Malawi na Tanzania kumaliza mvutano kuhusu Ziwa Nyasa

Ujumbe wa viongozi wa Malawi na Tanzania wameanza kikao chao hapo jana kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Mzuzu kujaribu kumaliza tofauti zilizoibuka hivi karibuni kuhusu mpaka wa ziwa Nyasa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Malawi Ephraim Mganda Chiume alikuwpo wakati wa ufunguzi wa kikako hicho.

Waziri huyo alisema kuwa wana imani kuwa mkutano wao wa siku tano utazaa matunda na kufikia muafaka kuhusu mpaka halali wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa hilo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania Bernad Membe imeelezwa hakuhudhuria mkutano huo lakini alituma wawakilishi ambapo anatarajiwa kuhudhuria siku ya mwisho ya mkutano.

Mgogoro kati ya nchi hizo mbili ulizuka baada ya kampuni ya Uingereza ya Surestream kuanza kufanya utafiti wake wa mafuta na gesi kaskazini mwa ziwa Nyasa kwenye eneo la Tanzania.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.