Pata taarifa kuu
SADC

Marais wa SADC kuijadili Zimbabwe na Madagascar

Mkutano wa marais wa mataifa ya Kusini mwa Afrika unafanyika Ijumaa hii mjini Maputo nchini Msumbiji kuijadili hali ya kisiasa nchini Madagascar na Zimbabwe. 

Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo mawili yapo katika harakati za kuandaa Uchaguzi Mkuu mwaka ujao ambao utakuwa kama kipimo cha kukomaa kwa demokrasia katika mataifa hayo na Muungano huo wa SADC.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekuwa nchini Zimbabwe kukutana na viongozi wa kisiasa nchini humo kushinikiza mabadiliko ya kisiasia nchini humo pamoja na kuhakikisha kuwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanyika mwaka huu kabla ya uchaguzi Mkuu.

Tofauti za kisiasa kati ya rais wa Madagascar Andry Rajoelina na rais wa zamani Marc Ravalomanana pia zinatarajiwa kuzungumziwa katika mkutano huo baada ya wanasiaisa hao kushindwa kupata suluhu chini ya mpatanishi wao, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kwa mara ya pili.

Madagascar inatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wake mkuu mwaka ujao na rais Rajoelina ambaye alimpindua Ravalomanana mwaka 2009 ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini hataki rais huyo wa zamani kusimama kwa sababu za kisiasa .

Rajoelina na Ravalomanana walipewa na Jumuiya ya mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC hadi Alhamisi tarehe 16 mwezi na Agosti wawe wamemaliza tofauti zao jambo ambalo huenda lisifanyike.

Mbali na mzozo huo wa kisiasa, Muungano huo utajadili mapendekezo ya Dola Milioni 500 ya kujenga barabara na reli kuunganisha mataifa hayo 15.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.