Pata taarifa kuu
NIGERIA

Watu 15 waripotiwa kuuawa kwenye shambulio lililolenga kanisa kaskazini mwa Nigeria

Watu kumi na tano wameripotiwa kuuawa nchini Nigeria kwenye mji wa Otite kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia mtu mmoja kuvamia kanisa moja na kuanza kuwafyatulia risasi waumini.

Wananchi wa Nigeria wakishuhudia moja ya shambulio kwenye kanisa kaskazini mwa nchi hiyo
Wananchi wa Nigeria wakishuhudia moja ya shambulio kwenye kanisa kaskazini mwa nchi hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, waltu wasiofahamika wakiwa wamevalia mavazi yaliyoficha nyuso zao walifika kwenye kanisa hilo na kuanza kufyatua risasi zilizopelekea pia kuuawa kwa mchungaji aliyekuwa akisalisha.

Luteni kanali Gabriel Olorunyomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kubaini ni watu gani ambao wamehusika kwenye shambulio hilo.

Hata hivyo taarifa za awali zinasema kuwa huenda watu waliotekeleza shambulio hilo wakawa ni wafuasi wa kundi la Boko Haram ambalo limeapa kutekeleza mashambulizi zaidi dhidi ya makanisa.

Mashambulizi hayo yameendelea kuongezeka ambapo siku ya jumapili kulifanywa shambulio jingine kama hilo kwenye jimbo la Kani kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu saba waliuawa na wengine kadhaa kujerihiwa.

Rasi wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametangaza vita na wafuasi wa kundi la Boko Haram ambapo ameagiza kuongezwa ulinzi kwenye miji ambayo kundi hilo linafanya shughuli zake na kufanya operesheni za nyumba kwa nyumba kuwasaka wapiganaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.