Pata taarifa kuu
Madascar

Mke wa Marc Ravalomanana awasili Madascar baada ya kuruhusiwa

Mke wa Rais aliyeng'olewa madarakani nchini Madagascar, Marc Ravalomanana amerejea nchini mwake baada ya yeye na mke wake kuzuiwa mara mbili kuingia nchini humo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Bi. Lalao Ravalomanana amewasili katika ardhi ya Madagascar na kuzuiwa kwa muda na maafisa wa serikali katika uwanja wa ndege lakini aliruhusiwa kuingia nchini humo baada ya waziri mkuu kumruhusu kwa njia ya simu.

Kureje kwa mke huyo wa Ravalomanana kumekuja baada ya mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Ravalomanana na Andry Rajoelina nchini Shelisheli.

Wakati viongozi mahasimu nchini Madagascar rais Andry Rajoelina na mwenzake Marck Ravalomanana wakimaliza mkutano wao bila kupatikana makubaliano rasmi, mazungumzo mapya yamepangwa kufanyika kabla ya kufikia muda wa mwisho uliowekwa na Umoja wa Afrika.

Viongozi hao walimaliza mkutano wao nchini Shelisheli kati kati ya wiki hii na kushindwa kuafikiana namna ya kumaliza tofauti zao.

Hata hivyo viongozi hao wamekubaliana kuandaa uchaguzi mwingine jambo ambalo linafanya kuwepo kwa mazungumo mengine kwenye siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.