Pata taarifa kuu
Madascar

Majeshi ya Madagascar yafanikiwa kuzima mapigano

Majeshi ya serikali ya Madagascar yametangaza kufanikiwa kuzima mapigano yaliyozuka kwenye kambi moja ya jeshi nchini humo na kwamba watu watatu waliuawa kwenye makabiliano hayo.

RFI/Marie Audran
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yalizuka baada ya afisa mmoja aliyetumwa kwenda kufanya mazungumzo na vikosi vya serikali kuuawa na kusababisha baadahi ya wanajeshi kuasi na kuanzisha mapigano hayo.

Msemaji wa jeshi la Madagascar Rarasoa Ralailomady amethibitisha kumalizika kwa jaribio la mapinduzi na kwamba hali ya usalama imerejea.

Kauli kama hiyo imetolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Omary Berzik ambaye amesema ulinzi umeendelea kuimarishwa kwenye nchi hiyo.

Mapambano hayo yanazuka wakati siku ya jumatano viongozi wanaohasimiana rais wa sasa Andy Rajoelina na mwenzake aliyepinduliwa Mark Ravalomanana wanatarajiwa kukutana kwa mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.