Pata taarifa kuu
LIBYA-UHOLANZI

Wajumbe wa Mahakama ya ICC wawasili Uholanzi baada ya kuachiwa huko Libya

Wajumbe wanne kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC ambao walikuwa wanashikiliwa nchini Libya tangu mwezi uliopita wakati walipomtembelea Seif Al Islam Gaddafi wamerejea nchini Uholanzi wakiwa salama baada ya kuachiwa hiyo jana.

Mwanasheria wa Mahakama ya ICC Melinda Taylor akiwa na wafanyakazi wenzie wakiwa wamerejea Uholanzi
Mwanasheria wa Mahakama ya ICC Melinda Taylor akiwa na wafanyakazi wenzie wakiwa wamerejea Uholanzi
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Mahakama ya ICC Fadi El Abdallah amesema wajumbe hao wote wanne wamewasili baada ya kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kufanya mawasiliano na Al Islam ili aweze kukubali kesi yake ihamishiwe katika mahaka hiyo badala ya kuendelea kusikilizwa nchini Libya.

Wajumbe hao wameachiwa baada ya kufanyika mazungumzo baina ya Viongozi wa serikali ya Libya na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya ICC Fatou Bensouda ambaye alizuru nchini humo katika kuendelea na juhudi za kuhakikisha wanaachiwa baada ya kuhukumiwa mwezi uliopita.

Wajumbe hao wa ICC waliachiwa kisha kusafiri hadi nchini Italia kabla ya kupanda ndege nyingine kuelekea Hague nchini Uholanzi na tayari wameshaungana na familia zao zilizokuwa na hofu juu ya usalama wa wajumbe hao baada ya kusekwa rumande.

Msemaji wa Mahakama ya ICC amesema wajumbe hao wanne baada ya kurejea wamepatiwa mapumziko kabla ya kurejea kuendelea na majukumu mengine ambayo yanawakabili katika Mahakama hiyo.

Wakili Melinda Taylor ambaye ni raia wa Australia pamoja na wenzake watatu ambao ni Helen Assaf, Alexander Khodakov na Esteban Peralta Losilla ambao walikamatwa katika Jimbo la Ziltan kwa kosa la kushukiwa kuingia gerezani kinyume cha utaratibu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Mohammed Abdel Aziz amesema wajumbe wa Mahakama ya ICC wameachiwa baada ya kufanyika kwa mazungumzo baina serikali na ujumbe kutoka Hague.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.