Pata taarifa kuu
MALI

Wapiganaji wa Ansar Dine wa nchini Mali waendelea kufanya uharibifu licha ya kutishiwa kufunguliwa Mashtaka na Mahakama ya ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC imetishia kuwachukulia hatua za kisheria Wapiganaji wa Kiislam waliopo Kaskazini mwa Mali kutokana na kuendelea kufanya uharibifu kulenga maeneo ambayo ni urithi na vivutio kwa utalii.

Baadhi ya maeneo ambayo yanaendelea kuharibiwa na Wapiganaji wa Kundi la Ansar Dine huko Timbuktu nchini Mali
Baadhi ya maeneo ambayo yanaendelea kuharibiwa na Wapiganaji wa Kundi la Ansar Dine huko Timbuktu nchini Mali
Matangazo ya kibiashara

Maeneo ambayo Mahakama ya ICC kupitia Mwendesha Mashtaka wake Fatou Bensouda wametishia kuyachukulia hatua kali za kisheria ni yale ambapo yapo katika eneo la Timbuktu ambalo kwa sasa limeanza kukabiliwa na uharibifu.

Maeneo hayo yamekuwa yakitumiwa kama vituo vya kitalii pamoja na sehemu za kihistoria ambazo zinaeleza kumbukumbua ya watawala waliopita wakati wa ukoloni lakini Ansar Dine wanaona maeneo hayo ni sawa na kuendelea kuabudu masanamu.

Bensouda amesema vitendo ambavyo vinafanywa na Wapiganaji wa Kiislam wa Ansar Dine ni sawa kabisa na uhalifu wa kivita na amewataka kama wanataka kuepuka mkono wa sheria waache mara moja uharibifu ambao wanaendelea kuufanya kwa sasa.

Kitisho cha Mahakama ya ICC kimeendelea kupuuzwa na Wapiganaji wa Kiislam wa nchini Mali wa Ansar Dine ambao wameshambulia na kuvunja lango la kuingia katika msikiti uliojengwa karne ya kumi na tano huko Timbuktu.

Msikiti huo unaotajwa kama kivutio kikubwa zaidi ya utalii kimeshambuliwa na Wapiganaji hao na kuongeza hofu ya kuharibiwa kwa sehemu zote ambazo zimekuwa ni kivutio kwa watalii ambao wamekuwa wakitembelea Timbuktu.

Kundi la Wapiganaji wa Ansar Dine limesema kuwa litaendelea kushambulia mabaki yote yakiwemo makaburi, masanamu na hata misikiti ambayo imekuwa ikitumika na watu kwenda kuabudu kitu kinachokwenda kinyume na imani ya Kiislam.

Ansar Dine wamesema watahakikisha wanashambulia kila eneo ambalo linaendelea kupigwa kelele na Jumuiya ya Kimataifa na hata wale ambao hawafuati imani ya kiislam inayokataza kuabudu masanamu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.