Pata taarifa kuu
Côte d’Ivoire

Viongozi wa Côte d’Ivoire wagundua njama za mapinduzi

Viongozi wa Côte d'Ivoire wamethibitisha kugundua njama za ma afisa wa zamani na wanasiasa wa utawala wa rais Laurent Gbagbo ya kutaka kuupindua utawala uliopo sasa wa rais Allasane Dramane Ouattara. Waziri wa mambo ya ndani Hamed Bakayoko amejitokeza jana kwenye luninga ya taifa ya nchi hiyo na kudai kuwa maafisa wa jeshi ambao bado wanaomuunga mkono rais wa zamani Laurent Gbagbo na wanasiasa ndio wanaohusika na mpango huo. Wanasiasa wa chama cha Laurent Gbagbo walio uhamishoni nchini Ghana, wametupilia mbali tuhuma hizo.

Rais wa Cote d'Ivoire Ouattara na waziri wa mambo ya ndani Hamed Bakayoko
Rais wa Cote d'Ivoire Ouattara na waziri wa mambo ya ndani Hamed Bakayoko AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

watu wa karibu na rais wa zamani Laurent Gbagbo wamesema huu ni mchezo wa kuigiza ambao serikali ya Ouattara inacheza baada ya kusikia uwezekano wa kuachiwa huru kwa muda rais wa zamani Laurent Gbagbo, hivyo kuonyesha kwamba nchi ipo hatarini, ili jaji wa mahakama ya ICC asimuache huru Laurent Gbagbo.

Jina la msemaji wa zamani wa rais Laurent Gbagbo Justin Katinan Kone linatajwa kuwa ndie kiongozi wa mpango huo wa mapinduzi. Akihojiwa na RFI, mtu ambae anatuhumiwa na vyombo vya sheria nchini Côte d'Ivoire kuhodhi pesa za benki ya mataifa ya Afrika magharibi BCEAO na kusema kwamba ni aibu kubwa sana kwa viongozi wa Côte d'Ivoire ambao wanataka kupaka tope upinzani, ambapo sio njia thabiti ya kuelekea katika maridhiano.

Waziri huyo wa zamani anahoji kuhusu hali ya kuzuiliwa na kuhojiwa kwa waziri wa zamani wa ulinzi Moise lida Kouassi kuliko pelekea kukiri kwake katika njama hizo. Na kusema kwamba viongozi wa Côte d'Ivoire wametuhumu mamluki wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo kuhusika katika mauaji yaliotokea magharibi mwa nchi hiyo, lakini Umoja wa Mataifa wao haujataja wahusika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.