Pata taarifa kuu
Somalia

Kundi la Al Shabab lakimbia ngome, mwandishi auawa Somalia

Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab lenye uhusiano na Mtandao wa Kigaidi wa Al-Qaeda lenye maskani yake nchini Somalia limekimbia ngome yake ya Afgoye kutokana na operesheni inayofanywa na Majeshi ya AMISOM kwa kushirikiana na Jeshi la Serikali.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa Jeshi la Somalia Jenerali Abdulaji Osman amesema wamekaribia kuimaliza ngome ya Wanamgambo wa Al Shabab iliyopo Afgoye na watamaliza operesheni hiyo muda si mrefu kutokana na kutokabiliwa na upinzani wowote.

Kamanda Osman amesema kutokabiliwa na upinzani kwa Jeshi lao ni ishara tosha kabisa Wanamgambo wa Al Shabab wamekimbia ngome yao kitu ambacho kimewafanya wapige hatua haraka zaidi tofauti na walivyofikiri awali.

Katika hatua nyingine Watu wenye silaha wamemuua mwandishi wa habari nchini Somalia Ahmed Ado Anshur katika Mji Mkuu Mogadishu na kufanya takwimu kuonesha huyu ni mwandishi wa sita kuuawa mwaka huu pekee wafanyakazi wenzake wamethibitisha.

Anshur ambaye alikuwa Mwandishi wa Habari wa Radio Shebelle ameuawa na watu wenye silaha wasiojulikana rafiki wake wa karibu Abdi Osmail ameeleza hilo ni tukio baya na linaongeza hofu kwa waandishi nchini humo.

Anshur anakuwa mwandishi wa habari watatu kuuawa kutoka Radio Shabelle na alifikwa na mauti wakati akirejea nyumbani kutoka kazini na hakuna sababu ambazo zimewekwa bayana kuwa chanzo cha kuuawa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.