Pata taarifa kuu
DRC

Watu 100 wauawa DRC katika kipindi cha wiki moja

Watu wasiopungua 100 wameuawa katika kipindi cha wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mapambano baina ya waasi wa kihutu wa Rwanda, FLDR na kundi la kijeshi la Mai Mai mashariki mwa nchi hiyo inayoongozwa na Joseph Kabila.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wanaharakati nchini humo kundi la Mai Mai liliwashambulia waasi wa FDRL ambao walikua wakimbulia watu wote waliokuwa mbele yao wakiwatuhumu kuwa walikua wanashirikiana na kundi la Mai Mai.

Mratibu wa shirika la kiraia la Kivu Kaskazini Omari Kavota amesema kuwa katika hatua nyingine kundi la Mai Mai ambalo lilikuwa likiwasaka FDRL nalo lilikua likiwalenga watu wote ambao wailikua wakiingia katika maeneo yao huku wakidai kuwa walikuwa ni washirika wa FDRL.

Miongoni mwa watu waliouawa katika kipindi cha juma moja lilopita ni raia na waluawa kwa visu na mapanga na hata kusababisha raia wengine kukimbia makazi yao.

Waasi wa FDRL wanawajumuisha wanajeshi waasi wa zamani waliofanya mauaji ya halaiki dhidi ya watusi wachache nchini Rwanda kunako mwaka wa 1994 na kukimbilia katika nchi jirani ya DRC.

Mauaji ya papo kwa papo yamekuwa yakiendelea katika mgogoro huo wa vikundi vya waasi walioko katika maeneo ya mikoa ya mashariki ya DRC huko Afrika ya Kati.

Aidha mapigano mengine yanayosababisha vifo yanafanyika katika jimbo la Kivu ya Kaskazini kati ya majeshi ya serikali ya DRC, maarufu kama FARDC na waasi wa zamani ambao baadaye waliingizwa katika majeshi ya serikali kama sehemu ya mpango wa amani wa mwaka 2009.

Hata waasi hao wameamua kujitoa katika majeshi hayo kwa madai ya malipo finyu na kukabiliwa na maisha magumu na sasa wanaendeleza uasi dhidi ya majeshi ya serikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.