Pata taarifa kuu
ALGERIA

Raia nchini Algeria washiriki zoezi la upigaji kura kuchagua wabunge

Raia nchini Algeria hii leo wameshiriki zoezi la upigaji kura za kuchagua wabunge kwenye uchaguzi ambao unatarajiwa kugubikwa na masuala mbalimbali ikiwemo watu kutojitokeza kupiga kura. 

Ahmed Ouyahia waziri mkuu wa Algeria
Ahmed Ouyahia waziri mkuu wa Algeria Reuters
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu milioni 22 wamejiandikisha kushiriki zoezi la upigaji kura ambapo watawapigia wabunge toka vyama 44 ambavyo baadhi yao vilisajiliwa mwaka huu.

Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika amewataka wananchi kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi huo ambao ameahidi kuwa utakuwa huru na haki na kwamba kila mwananchi ashiriki kumchagua kiongozi anayemtaka.

Licha ya Serikali kuahidi uchaguzi ulio huru na haki, lakini wachambuzi wa mambo wanadai kuwa huenda asilimia 35 ya wapiga kura wasijitokeze kwenye vituo vya kupiga kura ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2007.

Wachambuzi hao wameongeza kuwa, uchache wa watu kushiriki kwenye uchaguzi huo unatokana ukandamizwaji wa demokrasia uliokuwepo nchini humo kwa muda mrefu ambapo baadhi ya vyama vilikuwa haviruhusiwi kushiriki huku viongozi wake wengi wakiendelea kushikiliwa gerezani.

Takwimu zinaonyesha kuwa wananchi wengi hawatashiriki kupiga kura nchini humo katika kile kinachoonekana kuendelea kushinikiza Serikali iliyoko madarakani kuondoka na kuitisha uchaguzi mkuu mpya wa urais.

Rais Bouteflika ameahidi kufanyia mabadiliko katiba ya nchi hiyo ambayo wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakishinikiza kufanyika mabadiliko ya katiba kabla ya uchaguzi wa ubunge jambo ambalo serikali haijatekeleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.