Pata taarifa kuu
BLANTYRE-MALAWI

Joyce Banda aongoza maelfu ya wananchi wa Malawi kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Bingu wa Mutharika

Rais wa Malawi Joyce Banda hii leo amewaongoza maelfu ya wananchi kwenye ukumbi wa bunge la nchi hiyo kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bingu wa Mutharika. 

Marehemu Bingu wa Mutharika aliyekuwa rais wa Malawi
Marehemu Bingu wa Mutharika aliyekuwa rais wa Malawi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wananchi elfu tatu wameripotiwa kuhudhuria tukio hilo ambapo wengi wao walikuwa wakitokwa na machozi mara baada ya kuuona mwili wa kiongozi wao.

Mutharika alifariki dunia majuma kadhaa yaliyopita akiwa nchini Afrika kusini ambako alikwenda kupatiwa matibabu ya maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu kiongozi huyo.

Mwili wa Mutharika aliwasili nchini humo siku ya jumamosi ukitokea Afrika kusini ambapo shughuli za mazishi zinaendelea kwa wananchi kupata fursa ya kuuga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa.

Kiongozi huyo anatarajiwa kuzikwa jumatatu ijayo kijijini kwake nje kidogo ya mji wa Blantyre.

Marehemu Mutharika atakumbukwa kwa juhudi zake za kutokomeza umasikini nchini humo pamoja na kupambana na rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.