Pata taarifa kuu
MALI

Spika wa Bunge Nchini Mali kuapishwa kesho kuongoza Serikali ya mpito kabla ya kuitisha Uchaguzi

Spika wa Bunge Nchini Mali Dioncounda Traore anatarajiwa kuapishwa kesho kushika wadhifa wa Urais kuongoza serikali ya mpito kabla ya kuhitisha Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kutejesha Utawala wa Kiraia kufuatia Jeshi likiwa chini na Kepteni Amadou Haya Sanogo kumuangusha Rais Amadou Toumani Toure.

Spika wa Bunge Nchini Mali Dioncounda Traoré akiwa na Kiongozi wa Jeshi Kepteni Amadou Sanogo wakati wa mazungumzo ya kurejesha serikali ya kiraia
Spika wa Bunge Nchini Mali Dioncounda Traoré akiwa na Kiongozi wa Jeshi Kepteni Amadou Sanogo wakati wa mazungumzo ya kurejesha serikali ya kiraia AFP/HABIBOU KOUYATE
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kumuapisha Spika wa Bunge la Mali unakuja baada ya kupata baraka za Mahakama ya Katiba Nchini humo ambayo ilisajili rasmi na kisha kutambua kujiuzulu kwa Rais Toure kitu kinachotoa Mamlaka kwa Kiongozi huyo wa shughuli za bunge kuongoza serikali ya mpito kwa siku arobaini.

Kuapishwa kwa Spika Traore kunatajwa kuwa ni mwanzo wa kuingusha nchi ya Mali ambayo imeingia kwenye mgawanyiko mkubwa siku kadhaa baada ya Jeshi chini ya Kapteni Sanogo kuchukua utawala ambapo Waasi wa Tuareg na Makundi mengine ya Kiislam yakatangaza uhuru wa eneo la Azawad.

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka Bamako zinasema kuwa Spika huyo ataapishwa kabla ya kuanza kazi ya kuimarisha Utawala wa kirai sambamba na kuimarisha ushirikiano baina na wananchi wa Azawad na wale wa Bamako licha ya kushuhudiwa mgawanyiko mkubwa baina ya maeneo hayo mawili.

Juhudi za kurejesha serikali ya kiraia nchini Mali zimesimamiwa ipasavyo na Jumuiya ya UshirIkiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi ECOWAS zikiongozwa kwa ukaribu mkubwa na Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ambaye alisimamia mazungumzo baina ya Kepteni Sanogo na Rais Toure.

Rais Toure alifikia hatua ya kujiuzulu mwishoni mwa juma hili ikiwa ni sehemu ya mapngo wa kurejesha amani na utulivu katika nchi ya Mali baada ya kupitia kwenye msukosuko wa mapinduzi ya amani ambayo yalitoa nafasi kwa jeshi kushika hatamu kwa kisingizio serikali imeshindwa kupambana na Waasi wa Tuareg.

Katika hatua nyingine Kundi la Waislam wenye Msimamo nchini Nigeria Boko Haram limeyajwa kuwa mfadhili mkubwa wa Waasi wa Tuareg ambao wamejiimarisha Kaskazini mwa Mali na hata kufikia hatua ya kutangaza uhuru wa eneo la Azawad kitendo ambacho kimepingwa na Mataifa ya Magharibi.

Boko Haram wanatajwa kuwapa nguvu Tuareg kitu ambacho kinaonekana kinaweza kikatatiza juhudi za kurejesha amani ya kudumu katika nchi ya Mali wakati huu ambapo serikali ya mpito inatarajia kuanza kazi yake hiyo kesho huko Bamako.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.