Pata taarifa kuu
MalaWI

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika afariki dunia

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amefariki dunia kwa ugonjwa wa msituko wa moyo vimeeleza vyanzo kutoka katika hospitali moja nchini Afrika Kusini alikokimbizwa baada ya kupatwa na matatizo hayo ya moyo.

(CC)World Economic Forum/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo serikali ya nchini ilikuwa bado haijathibitisha kuhusu kifo cha rais huyo anayedaiwa kuiacha nchi yake katika hali ya wasiwasi kisiasa.

Vyanzo hivyo vya habari vilivyotoa taarifa za kifo cha Rais Bingu wa Mutharika vilizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina vimesema kuwa rais huyo alifariki baada ya saa mbili tangu kuanza kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Malawi, Makamu wa Rais Joyce Banda ndiye anatarajiwa kushika madaraka ya urais.

Rais wa Malawi Bingu Wa Mutharika alikua kwenye hali mbaya kiafya na alikuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali moja huko nchini Afrika Kusini baada ya kupata ghafla maradhi ya mshituko wa moyo.

Hali ya afya ya Rais Mutharika ilikua mbaya baada ya kuelezwa kuanguka akiwa katika makazi yake huko Lilongwe na kulazimika kupelekwa katika hospital ya Kamuzu na kisha baadaye hali ilipozidi kuwa mbaya akahamishiwa nchini Afrika Kusini.

Makamu wa Rais wa Malawi Joyce Banda ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya Rais Mutharika alithibitisha Kiongozi huyo kukabiliwa na maradhi ya shambulizi la moyo lililochangia kuanguka kwake.

Wananchi wa Malawi walitakiwa kuwa watulivu wakati ambao Rais Mutharika alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu huku wakishauriwa kuendelea kuombea Kiongozi wao ili apate nafuu haraka na kurejea nyumbani mapema hali ambayo imekuwa tofauti.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.