Pata taarifa kuu
Nigeria-Mauritania

Raia watatu wa Mauritania washikiliwa nchini Nigeria baada ya kushukiwa kuwa wafuasu wa Al Qaeda

Mamlaka nchini Nigeria inawashikilia watu watano akiwemo Raia wa Mauritania, wanaoamika kuwa wafuasi wa kundi la wanamgambo la Al Qaeda lililo na makazi yake kaskazini mwa Afrika. Kukamatwa kwa watu hao kumekuja kufuatia tukio la kutekwa nyara kwa Raia mmoja wa Ujerumani.

Picha zinazoonyesha kundi lenye mfungamano na Al Qaeda likiwashikilia mateka
Picha zinazoonyesha kundi lenye mfungamano na Al Qaeda likiwashikilia mateka AFP PHOTO/ANI
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa wanne walikamatwa juma lililopita kaskazini mwa mji wa Kano katika duka moja linalomilikiwa na Raia wa Mauritania.

Maafisa usalama walikamata kompyuta na silaha katika duka hilo halikadhalika walikamata nyaraka za Al Qaeda zinazoelezea taratibu za operesheni za kundi hilo, hali iliyodhihirisha kuwa washukiwa hao wana uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Mamlaka ya Nigeria imekuwa ikipata changamoto kubwa kutokana na matukio ya utekaji nyara na machafuko yanayosababishwa na kundi la Boko haram halikadhalika serikali hiyo ilikosolewa kwa kushindwa kuokoa mateka raia wa Italia na Uingereza ambao waliuawa na watekaji nyara kabla ya operesheni ya pamoja ya kuwaokoa kufanywa na kikosi cha usalama cha uingereza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.