Pata taarifa kuu
Mauritania

Mauritania yaridhia kumrudisha Libya Abdullah Senussi

Mauritania imeridhia kumpeleka Libya aliyekuwa mkuu wa maswala ya intelijensia nchini humo Abdullah Senussi ili kuyakabili mashtaka dhidi yake ya mauji yaliyotokea mwaka uliopita wakati wa harakati za mapinduzi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Libya Mustafa Abu Shagur amethibitisha uamuzi huo wa serikali ya Mauritania baada ya kufanya mashauriano na rais wa nchi hiyo Mohamed Ould Abdel Aziz.

Senussi mbali na kutakiwa kufunguliwa mashtaka ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya anatakiwa pia na Ufaransa halikadhalika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya mjini Hague nchini Uholanzi ICC.

Shagur amesema wameazimia kumrudisha senussi nchini Libya kwa kuwa amefanya uhalifu mkubwa dhidi ya raia wa Libya na ni lazima ajibu mashtaka mbele ya walibya, katika mahakama za libya.

Mbali na makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu ,Senussi anatakiwa kujibu shutma za kuhusika na udanganyifu, matumizi mabaya ya pesa ya uma na matumizi mabaya ya madaraka.

Senussi alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Nukchot siku ya Ijumaa juma lililopita alipoingia nchini humo akitokea Casablanca nchini Morocco akiwa na pasi ya kusafiria iliyoghushiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.