Pata taarifa kuu
Nigeria

Boko Haram yajiondoa katika mazungumzo na serikali ya Nigeria

Kundi la kigaidi la kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria, linasema halitashiriki tena katika mazungumzo na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi hilo Abul Qaqa, amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kugundua  kuwa serikali haileweki na "Mungu" amewaambia kuwa hakuna lolote litakalotokea katika mazungumzo yao na serikali kwa kile kundi hilo inasema haiaminiki.

Boko Haram ilikuwa imeiwekea sharti serikali kuwaachilia huru wanachama wake wote ili mazungumzo hayo yaendelee ,sharti ambalo halijafanyika kulingana na msemaji wa kundi hilo.

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya serikali na kundi hilo yamekuwa yakiendelea kimyakimya na yamekuwa katika hatua za mwanzo kujaribu kupata suluhu la kudumu kati ya serikali na Boko Haram.

Rais Goodluck Jonathan alinuia kutumia mazungumzo hayo kumaliza mashambulizi ya miezi kadhaa ambayo yamekuwa yakiendelea kaskazini mwa nchi hiyo hasa katika jimbo la Kano,na kundi hilo linalenga majengo ya usalama  na makanisa.

Hatua ya Boko Haram kuamua kujiondoa katika mazungumzo hayo ni pigo kwa serikali ya rais Jonathan,ambayo imeonekana kushindwa kutatua changamoto ya ukosefu wa usalama Kaskazini mwa nchi hiyo.

Boko Haram inasema inataka kuweka sheria za Kiislamu Kaskazini mwa nchi hiyo na kuligawa taifa hilo mara mbili Kaskazini liwe la waislamu na Kusini la Wakiristo.

Wachambuzi wa maswla ya usalama hata hivyo wanaona kuwa kukamatwa kwa wanachama na viongozi kadhaa wa kundi hilo katika siku za hivi karibuni kumedhoofisha kundi hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.