Pata taarifa kuu
LIBYA

Amnesty International yataka NATO kuchunguza mauaji ya raia nchini Libya mwaka uliopita

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linataka muungano wa majeshi wa nchi za magharibi NATO, kuchunguza mauji ya raia yaliyotokea nchini Libya wakati wa mashambulizi ya angaani dhidi ya wapiganaji wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo aliyeuawa kanali Muamar Gaddafi mwaka uliopita.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International pia inataka familia za wale wote watakaobainika kuwa waliuawa kwa mashambulizi hayo ya NATO, zifidiwe na majeshi hayo.

Shirika hilo linasema kuwa lina ushahidi wa visa 55 vya mauji ya raia vilivyotokana na mashambulizi hayo, wakiwemo watoto 16 na wanawake 14 waliuawa katika miji ya Tripoli, Zliten, Majer, Sirte na Brega.

Mashambulizi ya majeshi ya NATO yalisaidia kumalizika kwa uongozi wa Gaddafi na kusaidia baraza la mpito nchini Libya NTC kuchukua uongozi wa taifa hilo.

Urusi, Uchina, Afrika Kusini na India ni miongoni mwa mataifa ambayo yalishtumu NATO kukiuka  azimio la Umoja wa Mataifa na kuanza kufanya mashambulizi ambayo yaliungwa mkono na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa kile walichokisema yalinuwiya kuwalinda raia wa Libya.

Kwingineko, Libya inaomba kukabidhiwa kwa aliyekuwa mkuu wa Intelijensia wakati wa utawala wa Marehemu Kanali Mouamar Gaddafi nchini Libya, Abdullah Al Senussi baada ya kukamatwa nchini Mauritania.

Msemaji wa  Serikali mpya mjini Tripoli amesema kuwa Jenerali Senussi akabidhiwe nchini Libya kwa ajili ya kushtakiwa.

Senussi pia anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC akishutumiwa kuhusika na makosa ya Uhalifu dhidi ya Ubinadamu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.