Pata taarifa kuu
Algeria

Mahakama nchini Algeria yatoa hukumu ya Kifo kwa watu 16

Mahakama nchini Algeria imetoa hukumu 16 za kifo siku ya Jumanne na Jumatano kwa Watu 18 waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na Mashambulio ya Mabomu yaliyokuwa yakitekelezwa mwaka 2007 na kundi la Wanamgambo la Al Qaeda.

Wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda
Wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda
Matangazo ya kibiashara

Hukumu 9 za kifo zilitolewa siku ya jumanne, ikiwemo hukumu moja dhidi ya Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa Al qaeda kaskazini mwa Afrika la AQIM, na saba walihukumiwa siku ya Jumatano.
 

Wawili kati ya watuhumiwa hao walihukumiwa vkifungo cha miaka mitatu mpaka 10
Hukumu hiyo imekuja baada ya kuthibitishwa kuwa walishiriki katika mashambulio matatu ya Bomu la tarehe 11 Mwezi Aprili Mwaka 2007 ambapo watu 20 walipoteza maisha na wengine 222 kujeruhiwa.
 

Kundi la wanamgambo la AQIM linaendelea na Operesheni zake nchini Niger, Mali na Mauritania lakini uongozi umetawaliwa na Raia wa Algeria, kundi hili lilianza miaka ya 1990 likiwa na lengo la kuangusha serikali ya Algeria na kuunda Serikali ya Kiislam.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.