Pata taarifa kuu
Zambia

Chama cha MMD nchini Zambia kupinga Uamuzi wa Msajili wa Vyama Mahakamani

Rais wa zamani wa Zambia, Rupia Banda hii leo amesema kuwa uamuzi wa kufutwa kwa Chama chake kilichowahi kutawala Nchi hiyo cha Movement for Multi-Party Democracy, MMD ulikuwa wa makosa na kwamba uamuzi huo umenyang'anya Uhuru wa Watu. 

Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda
Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya Habari siku moja baada ya Chama cha MMD kufungiwa kwa kushindwa kulipa Ada ya Usajili,Rupia Banda amesema yeyote aliyehusika katika kukifunga Chama hicho amekosea.

Kwa mujibu wa Msajili wa vyama, chama cha MMD kinadaiwa kiasi cha Dola za Mrekani 74,300, Ada ambayo haikulipwa tangu Mwaka 1993.

Chama hicho kinachoelekea kupoteza Viti vyake vya ubunge 53 kimeapa kupinga uamuzi huo Mahakamani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.