Pata taarifa kuu
Niger

Zaidi ya watu milioni sita Nchini Niger wahitaji msaada kupambana na janga la njaa

Zaidi ya watu milioni sita nchini Niger wanahitaji msaada wa haraka wakati huu ambapo nchi hiyo ikiwa na tatizo la upungufu mkubwa wa Chakula kutokana na Ukame na visababishi vingine,shirika linaloshughulikia maswala ya chakula, Oxfam na UN limethibitisha.

Kamishna kutoka Shirika linaloshughulikia maswala ya Chakula, Fode Ndiaye
Kamishna kutoka Shirika linaloshughulikia maswala ya Chakula, Fode Ndiaye
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa maswala ya haki za Binaadam kutoka UN, Fode Ndiaye amesema kuwa hali za wanawake na watoto zinafifia haraka sana na kuomba jumuia ya Kimataifa kufanya kila liwezekanalo kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
 

Ndiaye amesema ili kuweza kukabiliana na tatizo la upungufu wa Chakula, Familia zinalazimika kupunguza kiasi cha chakula wanachokula kila siku, wanauza samani zao halikadhalika wengine huyahama makazi yao na kwenda Nchi jirani.
 

Baadhi ya jamii katika mji wa Tillabery, zaidi ya asilimia 40 ya wakazi wake wameviacha vijiji vyao mapema kwa ajili ya kutafuta chakula na makazi katika maeneo ya Mjini.
 

Nchini Niger, zaidi ya watoto 33,000 wameondolewa shuleni kwa sababu ya kuhama hama kwa wazazi, halikadhalika kwa ajili ya kusaidia kupatia mapato Familia zao, huku ikielezwa kuwa zaidi ya nusu milioni ya watoto wako kwenye hatari ya kuacha shule kutokana na tatizo la ukosefu wa Chakula.
 

Matatizo ya Ukame, kupanda kwa gharama za Chakula, Mazao duni, Umasikini na Migogoro vinatishia kuwepo kwa ukosefu wa Chakula katika mataifa ya Kaskazini mwa Afrika, zikiwemo, Chad, Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na kaskazini mwa Senegal.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.