Pata taarifa kuu
NIGERIA

Serikali ya Nigeria yasema bado iko radhi kufanya mazungumzo na kundi la Boko Haram

Serikali ya Nigeria kupitia kwa waziri wa habari wa nchi hiyo Labaran Maku imesema kuwa bado iko tayari kufanya mazungumzo na wapiganaji wa kudni la Boko Haram ambao wameendelea kufanya mashambulizi dhidi ya raia. 

Polisi nchini Nigeria wakiwa kwenye moja ya eneo ambalo Boko Haram walitekeleza shambulio lao
Polisi nchini Nigeria wakiwa kwenye moja ya eneo ambalo Boko Haram walitekeleza shambulio lao Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema kuwa Serikali bado inatoa nafasi kwa viongozi wa kundi hilo kurejea kwenye meza ya mazungumzo kujaribu kutafuta suluhu ya machafuko ambayo yanazidi kushuhudia mamia ya wananchi kaskazini mwa nchi hiyo wakipoteza maisha.

Kundi la Boko Haram lenyewe mpaka sasa halijasema lolote kuhusu uwezekano wa viongozi wake kukutana na Serikali ya Nigeria kwa mazungumzo huku waiapa kuendeleza mashambulizi.

Kundi hilo limekuwa likipinga elimu ya magharibi kufundishwa nchini humo likidai kuwa inaenda kinyume na misingi ya dini ya kiislamu ambapo wananchi wengi wa Kaskazini mwa nchi hiyo ni waislamu.

Mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakilenga vituo vya Polisi na makanisa kwa lengo la kuionyesha Serikali kuwa linachukizwa na mfumo wa kimagharibi ambao umeanza kuingizwa nchini humo.

Rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan ameendelea kutoa wito kwa viongozi wa kundi hilo kukubali kutejea kwenye meza ya mazungumzo kujadili ni kitu gani wanataka na kama kunauwezekano wa madai yao kutekelezwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.