Pata taarifa kuu
NIGERIA-LIBERIA

Wakimbizi wa Liberia waishio Nigeria wapewa muda kurejea makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limetoa muda kwa wahamiaji kutoka nchini Liberia waishio nchini Nigeria kurejea makwao kwa hiari ifikapo katikati mwa mwaka huu.

Shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR lawataka raia wa Liberia walioko Nigeria kurejea makwao
Shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR lawataka raia wa Liberia walioko Nigeria kurejea makwao
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesisitiza wahamiaji hao kuhama vinginevyo watatambulika rasmi kama wakimbizi nchini Nigeria.

Wahamiaji wapatao elfu tano kutoka nchini Liberia ambao baadhi yao wanaishi nchini Nigeria tangu miaka ya 90 baada ya kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao,wanaendelea kuishi Nigeria hadi sasa.

Mwakilishi wa UNHCR nchini Nigeria amesema kuwa baadhi ya wahamiaji hawataki kurejea nchini mwao kutokana na kuhofia usalama ingawa amesisitiza kuwa ifikapo July Mosi mwaka huu wahamiaji ambao hawatakuwa wamejisajili kwenye mpango wa kurejea nyumbani kwa hiari watapoteza haki ya kuwa wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.