Pata taarifa kuu
Côte d’Ivoire

ICC yatangaza hatuwa ya kuongeza muda wa uchunguzi juu ya kesi ya uhalifu wa kivita nchini Côte d’Ivoire

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC imetangaza hatua ya kuongeza muda zaidi wa uchunguzi juu ya kesi ya uhalifu wa kivita nchini Cote D'Ivoire iliyochangiwa na kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka elfu mbili na mbili.

Shamra shamra za uchaguzi nchini Cote d'Ivoire
Shamra shamra za uchaguzi nchini Cote d'Ivoire
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo unaelezwa utamlenga Rais wa zamani Laurent Gbagbo ambaye kwa sasa anakesi ya kujibu mbele ya Mahakama ya ICC lakini pia watakaokumbwa na uchunguzi huo ni pamoja na wafuasi wa rais wa sasa Alassane Dramane Ouattara.

Gbagbo alikamatwa kutokana na kutuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu wa kivita ambayo yalitokea baada ya kugoma kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais dhidi ya Mpizani wake Rais Ouattara.

Laurent Gbagbo alipelekwa kwenye mahakama ya uahalifu wa kivita ICC ilioko Uholanzi tangu Novemba mwaka 2011. kiongozi huyo anakabiliw ana makosa manne ya kujibu juu ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.